Friday, October 20, 2017

TAMASHA KUBWA LA UZINDUZI WA ALBAMS ZA NEEMA NG'ASHA SASA LIMEKARIBIA.

 


Muimbaji wa nyimbo za  Injili Neema Ng'asha kutoka jijini ,Mwanza  ameanza rasmi leo kutangaza mtandaoni uzinduzi wake mkubwa utakaofanyika tarehe 10/12/2017 katika uwanja wa CCM KIRUMBA,Mwanza.Neema Ng'asha akiongea na mwandishi wetu amesema anamshukuru sana Mungu kwa hatua hii aliyoifikia. Album zitakazo zinduliwa siku hiyo ni TUNAE BWANA DVD na USILIE TENA audio CD.Waimbaji binafsi wengi kutoka jijii Mwanza na kwaya zimethibitisha kuwepo katika uzinduzi huu.Neema amewaomba wakazi wa jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla wasikose kufika uwanjani siku hiyo maana Mungu atakwenda kuwahudumia kwa njia ya tofauti na pia anaomba waje kumtia moyo kununua kazi zake.
 

Wednesday, September 13, 2017

VIDEO YA "MATENDO YAKO" YA NEEMA NG'ASHA SASA IKO YOUTUBE
Muimbaji wa nyimbo za Injili Neema Ng'asha  ambaye kwa sasa anaishi jijini Mwanza,ameshaachia video yake mpya ya"MATENDO YAKO" katika mtandao wa youtube hivi karibuni.Wimbo wa "MATENDO YAKO"ni wimbo unaotukumbusha kumshukuru MUNGU kwa matendo yake makuu anayofanya kila siku maishani mwetu.Matendo ya MUNGU ni mengi sana mishani mwetu hata tukisema tuyahesabu hayahesabiki.
Neema anasema anamshukuru MUNGU wimbo huu umekuwa Baraka kwa watu wengi.
Video ya MATENDO YAKO imefanywa na director JAYMENGE wa kampuni ya Calmmedia kutoka Nairobi,Kenya.

Kutazama video hii bonyeza hiyo link ya blue hapo chini.https://www.youtube.com/watch?v=OzZcM2YyNxQ

Tuesday, August 15, 2017

VIDEO YA NEEMA NG'ASHA "MATENDO YAKO" KUPATIKANA YOUTUBE HIVI KARIBUNI.Muimbaji wa nyimbo za injili Neema Ng'asha anayeishi jijini Mwanza kwa sasa.anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kufanya video mbili za nyimbo "MATENDO YAKO " na "NAKUPENDA YESU".Video hizi zimefanywa na madirector Jay Menge na Josh Berry kutoka kampuni ya Calmmedia kutoka jijini Nairobi,Kenya. Neema Ng'asha amesema namshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii ya kipekee kwa kufanya kazi hii na kampuni ya Calmmedia kutoka Nairobi ,Kenya anasema huu utakuwa mlango wa ufikia hatua kubwa katika huduma yake.Director Jay Menge amesema kwa sasa tutaoa video moja ya "MATENDO YAKO" ambao itakuwa youtube hivi karibuni.Na amewaambia wadau wote wa muziki wa Injili Africa Mashariki kukaa mkao wa kuipokea video hii ambayo imekuwa na viwango vya juu kwa UTUKUFU WA MUNGU  na itafanyika Baraka kwa watu wengi watakao itazama.
 


 Muimbaji Boaz Anthony na Gloria Mbaruku wakiwa location.

Neema Ng'asha akiwa location.

Monday, June 19, 2017

VIDEO YA #USILIE TENA# YA NEEMA NG'ASHA SASA IPO YOU TUBE.

Muimbaji wa nyimbo za injili Neema Ng'asha kutoka jijini,Mwanza ameachia video yake ya wimbo wa #USILIE TENA# katika mtandao wa you tube tar 19/6/2017.Neema Ng'asha  amesema anamshukuru Mungu kazi yake imetoka vizuri na mpaka sasa watu wengi wameshaingia kwenye mtandao wa you tube kungalia video hii.Wimbo huu umefanyika Baraka kwa watu wengie sana maana unawatia moyo watu wasikate tamaa wamtazame YESU maana anaweza hakuna jambo gumu kwake.Video ya #USILIE TENA# imetengenezwa  na director Fred Mwamakula wa kampuni ya Mwamakula Production kutoka jijini Dar-es-Salaam.Kuangalia video hii naomba ubonyeze link hii,

https://www.youtube.com/watch?v=COF4kNaoTns&feature=youtu.be

Saturday, June 10, 2017

WIMBO WA "USILIE TENA" KUACHILIWA YOU TUBE TAR 15/6/2017.

Muimbaji wa nyimbo za Injili Neema Ng'asha kutoka jijini,Mwanza anatarajia kuachia video yake mpya katika mtandao wa you tube tar 15/6/2017.Neema Ng'asha anasema anamshukuru sana MUNGU kwa hatua hii aliyoifikia ya kutoa video hii,wimbo wa "USILIE TENA" ulisikika kwa mara ya kwanza mwaka jana katika vyombo vya habari mbalimbali hapa inchini .Wimbo huu umefanyika Baraka sana kwa watu wengi na wamekuwa wakiulizia video yake.
Muimbaji Neema anaomba watu wote wanaopenda kufuatilia kazi zake wasisahau kuingia you tube kusbscribe ili wafahamu kila kitu kinachoendelea kuhusu huduma yake.

Monday, May 22, 2017

NEEMA NG'ASHA KUIMBA TAMASHA LA PASAKA MWANZA.

Muimbaji wa nyimbo za injili Neema Ng'asha.
 
Muimbaji wa nyimbo za Injili Neema Ng'asha kwa mara ya kwanza alipata kibali kuimba kwenye tamasha la pasaka linaolandaliwa na kampuni ya MSAMA PROMOTIONS lililofanyikia jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba,Neema Ng'asha  anasema "amemuona Mungu akimsaidia sana mpaka kufikia hatua hii,siku hiyo ilikuwa ya kihistoria katika huduma yake  na alimuona Mungu akimpa kibali kikubwa kwa watu waliokuwa uwanjani pale".

WIMBO WA NAKUPENDA YESU WAFANYIKA FARAJA KWA WATU WENGI.


Namshukuru Mungu kwa Neema yake ameniwezesha kutoa wimbo mpya unaoitwa "NAKUPENDA YESU".Namshukuru Mungu kwa ajili ya huu wimbo umekuwa baraka kwa watu wengi kila nikisimama kuimba watu wanaguswa na pia wanaosilikiliza  Mungu amekuwa akiwahudumia.Wimbo huu unaelezea upendo wa Yesu jinsi alivyojitoa kwa ajili yetu alikubali kuacha enzi yake alidharauliwa na kukataliwa ili mimi na wewe tupate uzima.Wimbo huu uko kwenye album inayoitwa "USILE TENA"ambayo itakuwa tayari hivi karibuni katika mfumo wa DVD.kusikiliza huu wimbo fungua hii link https://youtu.be/YjA6BdYhtU8 .
Kwasasa nimehamia jijini Mwanza kwa hiyo watumishi mlioko jijini Mwanza msisite kunitafuta kwa ajili ya kuja kufanya huduma moyo wangu una shauku kubwa ya kumtumikia Mungu.mnaweza kuwasiliana na mimi kupitia facebook natumia jina Neema Ng'asha.