About Me

My photo
My Name is Neema Ng'asha C.E.O and Founder member of Strong Women Foundation.(SWF).

Thursday, January 24, 2019

NEEMA NG'ASHA ALAMBA DILI NZALI NEXT LEVEL PROMOTION.

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini,Mwanza Neema Ng'asha ameingia mkataba wa kusimamiwa kazi zake za uimbaji na kampuni ya NZALI NEXT LEVEL PROMOTION iliyoko nchini Marekani. Akiongea na mwandishi wetu Neema Ng'asha anasema anamshukuru sana MUNGU kwa hatua hii aliyofikia sababu lilikuwa ni ombi lake la muda mrefu sana. Neema Ng'asha anasema "NIMEJIFUNZA KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA" anazidi kusema amepitia changamoto nyingi sana ambazo bila msaada wa Mungu asingeweza kuendelea na huduma.Lakini leo anasema amemuona MUNGU akifanya njia pasipo na njia.
Neema Ng'asha anapenda kuwatia moyo waimbaji wengine wanaonza huduma wasikatishwe tamaa na mazingira magumu wanayopitia"WAMTEGEMEE MUNGU KWA MAJIRA NA WAKATI WAKE HUFANYA KILA KITU KWA UZURI"
Neema anapenda kumshukuru meneja wake Leonard Nzali  ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Marekani, kwa kumpa nafasi hii kufanya nae kazi ili kulitangaza neno la Mungu liwafikie watu wengi.

No comments:

Post a Comment