About Me

My photo
My Name is Neema Ng'asha C.E.O and Founder member of Strong Women Foundation.(SWF).

Tuesday, June 19, 2018

NEEMA NG'ASHA AACHIA VIDEO YA NAAMINI.

Kwa mara nyingine kutoka jijini Mwanza,Tanzania, Muimbaji wa nyimbo za injili Neema Ng'asha ametoa video yake mpya kabisa ya wimbo wa "NAAMINI"
Akizungumza na mwandishi wetu Neema Ng'asha anasema anamshukuru Mungu sana kwa hatua hii aliyofikia anasema "HATA SASA MUNGU NI EBENEZA KWANGU"Neema anaendelea kusema anazidi kumuona MUNGU kila siku akimtoa hatua moja kwenda nyingine haijalishi anakutana na vikwazo gani lakini MUNGU amekuwa mwaminifu kutimiza ahadi zake.
Wimbo wa "NAAMINI" ni wimbo unaotukumbusha kukokukata tamaa haijalishi tunapitia mapito gani.Kuna wakati tunapitia mambo magumu na tunakosa faraja kutoka hata kwa watu wetu wa karibu tunajiona tuko peke yetu,lakini ukweli ni kwamba MUNGU yuko pamoja nasi haijalishi tunapitia wapi atafanya mlango wa kutokea na kutupa ushindi.
Neema Ng'asha anasema anamshukuru MUNGU mpaka sasa video hii tayari imeshasambaa katika website nyingi ,blogs na  tayari umeshaanza kurushwa kwenye Television mbalimbali.Neema anasema anamshukuru sana Mungu  watu wameupokea vizuri wimbo na unaendelea kuwahudumia pia yuko tayari kwa mialiko.

Kutazama video hii bonyeza link ya blue hapo chini.







1 comment:

  1. i am very grateful to you for the information. I have used it.
    gclub

    ReplyDelete