Habari Njema kutoka jijini Mwanza kwa mara ya kwanza katika mwaka 2020 tumekusogezea wimbo mpya wa kuabudu unaoitwa UMEINULIWA kutoka kwa Neema Ng’asha.
Karibu kusikiliza wimbo huu mzuri na hakika utabarikiwa na kuinuliwa, Eimen.
Kutoka Tanzania kwa mara nyingine tena tumekusogezea wimbo mpya wa
kuabudu kutoka kwa Neema Ng’asha mwimbaji wa nyimbo za Injili akitokea
jijini Mwanza. Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri ambao kwa hakika utakubariki, Amen.
Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jiji Mwanza,Neema Ng'asha anatarajia kufanya tamasha la kusifu na kuabudu(IN HIS PRESENCE LIVE CONCERT SEASON ONE) ambapo siku hiyo atazindua album ya "AKISEMA NDIYO".Tamasha hilo litafanyika tarehe/2019 Katika kanisa la MICC,Nyegezi kwa Dr.Zakayo Nzogere.Neema Ng'asha amewakaribisha Wadau wote wa muziki wa injili kuja kwa wingi kumuabudu Mungu kwa pamoja.Waimbaji wengi wamethibitisha kuwepo siku hiyo kumtia moyo Neema Ng'asha.
Kwa mara nyingine tena muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza,Neema Ng'asha anatarajia kuachia kazi yake mpya iliyo katika mfumo wa audio inayoitwa"NI WAKO" Neema Ng'asha ambaye kwa sasa nafanya kazi chini ya usimamizi wa NZALI NEXT LEVEL PROMOTION amesema kazi hiyo itakuwa tayari hivi karibuni kwa hiyo anaomba wadau wote wa nyimbo za injili wafatilie katika youtube account yake"Neema Ng'asha na Youtube account ya Nzali Next Level pia katika ukurasa wa facekoob wa Neema Ng'asha na Nzali Leonard. Wimbo wa"NI WAKO" Umefanywa na Producer Ben William kutoka studio za APEX MUSIC, Mwanza.
Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini,Mwanza Neema Ng'asha ameingia mkataba wa kusimamiwa kazi zake za uimbaji na kampuni ya NZALI NEXT LEVEL PROMOTION iliyoko nchini Marekani. Akiongea na mwandishi wetu Neema Ng'asha anasema anamshukuru sana MUNGU kwa hatua hii aliyofikia sababu lilikuwa ni ombi lake la muda mrefu sana. Neema Ng'asha anasema "NIMEJIFUNZA KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA" anazidi kusema amepitia changamoto nyingi sana ambazo bila msaada wa Mungu asingeweza kuendelea na huduma.Lakini leo anasema amemuona MUNGU akifanya njia pasipo na njia. Neema Ng'asha anapenda kuwatia moyo waimbaji wengine wanaonza huduma wasikatishwe tamaa na mazingira magumu wanayopitia"WAMTEGEMEE MUNGU KWA MAJIRA NA WAKATI WAKE HUFANYA KILA KITU KWA UZURI" Neema anapenda kumshukuru meneja wake Leonard Nzali ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Marekani, kwa kumpa nafasi hii kufanya nae kazi ili kulitangaza neno la Mungu liwafikie watu wengi.
Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Mwanza,Neema Ng'asha kwa mara nyingine ametoa video mpya inayoitwa KHERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA ambayo imefanywa na Director IPMAGERA wa Smart Vision International.
Kutazama video hii bonyeza link hii 👇👇👇👇👇