About Me

My photo
My Name is Neema Ng'asha C.E.O and Founder member of Strong Women Foundation.(SWF).

Wednesday, January 4, 2017

ALBUM YA TUNAE BWANA SASA IKO SOKONI.

Napenda kumshukuru Mungu sana kwa kunisaidia kufanikisha kuweka wakfu album ya "TUNAE BWANA" tar 31/12/2016 (usiku wa mwaka mpya) ibada ya kuweka wakfu album ilifanyika kanisa DCT -Tabata shule ambapo katibu mkuu wa TAG Pastor Ron Swai aliombea na kuiweka wakfu album hii ili ikawe baraka kwa mwili wa KRISTO.Pia nilimshukuru Mungu kwa kuniongeza mwaka mwingine najua ni kwa Neema yake tu niko hai hadi leo ili nitimize kusudi lake.
Album hii inapatikana katika duka la Mwamakula Production-Dar-es-Salaam,mtaa wa masasi kwa masiliano piga 0673527249,kwa walio mkoani mnaweza kuipata kwa kupiga hiyo namba.Usikose copy yako.
                                        Pastor Ron Swai akizindua album ya TUNAE BWANA.





No comments:

Post a Comment