About Me

My photo
My Name is Neema Ng'asha C.E.O and Founder member of Strong Women Foundation.(SWF).

Monday, May 22, 2017

WIMBO WA NAKUPENDA YESU WAFANYIKA FARAJA KWA WATU WENGI.


Namshukuru Mungu kwa Neema yake ameniwezesha kutoa wimbo mpya unaoitwa "NAKUPENDA YESU".Namshukuru Mungu kwa ajili ya huu wimbo umekuwa baraka kwa watu wengi kila nikisimama kuimba watu wanaguswa na pia wanaosilikiliza  Mungu amekuwa akiwahudumia.Wimbo huu unaelezea upendo wa Yesu jinsi alivyojitoa kwa ajili yetu alikubali kuacha enzi yake alidharauliwa na kukataliwa ili mimi na wewe tupate uzima.Wimbo huu uko kwenye album inayoitwa "USILE TENA"ambayo itakuwa tayari hivi karibuni katika mfumo wa DVD.



kusikiliza huu wimbo fungua hii link https://youtu.be/YjA6BdYhtU8 .
Kwasasa nimehamia jijini Mwanza kwa hiyo watumishi mlioko jijini Mwanza msisite kunitafuta kwa ajili ya kuja kufanya huduma moyo wangu una shauku kubwa ya kumtumikia Mungu.mnaweza kuwasiliana na mimi kupitia facebook natumia jina Neema Ng'asha.

No comments:

Post a Comment