About Me

My photo
My Name is Neema Ng'asha C.E.O and Founder member of Strong Women Foundation.(SWF).

Sunday, January 19, 2025

Muimbaji wa Nyimbo za injili Neema Ng'asha aanzisha media inayoitwaGOSPEL VIBES MEDIA

 Kutoka jijini Mwanza Muimbaji wa nyimbo za injili Neema Ng'asha media inayoitwa GOSPEL VIBES MEDIA.Akiongea na mwandishi wa blog hii Neema Ng'asha ambaye ndiye Mkurugenzi mtendaji wa GOSPEL VIBES MEDIA amesema kumekuwepo na changamoto ya muda mrefu hasa jijini Mwanza waimbaji kupata huduma ya Digital marketing.Toka siko poa kusambaza CD lilipokufa Tanzania,waimbaji wengi wamepata changamoto kusambaza kazi zao ili kuwasifia watu wengi.Kwa sasa mtandao ndiyo chombo pekee kinachotumiwa na watu wengi duniani hivyo basi kuna ulazimu wa waimbaji kujua jinsi ya kutumia mtandao kusambaza kazi zao.Hivyo basi tunamshukuru Mungu kutusaidia kufungua media tukishirikiana na  Director IP Magera  kwa pamoja tunaamini media hii italeta mapinduzi makubwa siyo Mwanza tu hata Tanzania kwa ujumla.

Hivyo tunawakaribisha waimbaji na wachungaji kufanya kazi na sisi ili kuleta maongezeko kwenye huduma zenu.Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba 0754220078.

No comments:

Post a Comment