Neema Ng'asha,ni Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania. alianza kuimba tangu akiwa mtoto Sunday school.
Lakini ilipofika mwaka 1998 akiwa kidato cha pili Mungu alimupaka mafuta baada ya kushukiwa na Roho Mtakatifu kwa nguvu sana, tangu hapo akaanza kutunga nyimbo za injili.
Akaanzisha band iliyoitwa Jerusalem band ambayo walikuwa wakiimba na dada yake Martha Ng'asha na vijana wengine pale kanisani.
Baada ya kumaliza chuo pale AVU-University of Dar es salaam ,mwaka 2010 alingia studio na kurekodi album yake ya kwanza iliyoitwa USINIPITE MWOKOZI.
Mpaka sasa amerekodi album 3 na single nyingi ikiwemo SALAMA aliyoichia Mwezi March 2025.
Safiiii Sana na Hongera Mungu akuinue zaidi
ReplyDeleteAmina barikiwa
ReplyDelete